Deuteronomy 5:12-15

12 aAdhimisha siku ya Sabato na kuiweka takatifu, kama Bwana Mwenyezi Mungu wako alivyokuagiza. 13Kwa siku sita utafanya kazi na kutenda shughuli zako zote. 14 bLakini siku ya Saba ni Sabato kwa Bwana, Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yoyote, wewe, wala mwanao au binti yako, wala mtumishi wa kiume au mtumishi wa kike, wala ng’ombe wako, punda wako au mnyama wako yeyote, wala mgeni aliyeko malangoni mwako, ili kwamba mtumishi wako wa kiume na wa kike wapate kupumzika kama wewe. 15 cKumbuka mlikuwa watumwa huko Misri, na Bwana Mwenyezi Mungu wenu aliwatoa huko kwa mkono wenye nguvu na kwa mkono ulionyooshwa. Kwa hiyo Bwana Mwenyezi Mungu wako amekuagiza kuiadhimisha siku ya Sabato.
Copyright information for SwhKC